• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa falme za Kiarabu wapinga kujilinda kibiashara na kuunga mkono biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-04-03 09:08:18

    Umoja wa Falme za Kiarabu ikiwa ni nchi iliyo wazi, imesema inaunga mkono kufanya biashara iwe wazi na kupinga kujilinda kibiashara.

    Naibu waziri wa biashara ya kimataifa wa nchi hiyo Bw. Abdullah Al Saleh amesema hayo wakati akiwafahamisha wanahabari kuhusu mkutano wa 8 wa uwekezaji wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 April mjini Dubai.

    Amesema kuondoa vizuizi vya kibiashara imekuwa ni sera ya pamoja ya Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba GCC, ambalo Umoja wa Falme za Kiarabu ni nchi mwanachama.

    Bw. Al Saleh ametoa kauli hiyo kufuatia hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Marekani kuongeza ushuru kwa baadhi ya bidhaa kutoka nchi za nje, na kuleta hofu ya kuanza kwa vita ya biashara kati ya nchi kubwa duniani, ikiwa ni pamoja na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako