• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan atoa mwito kupambana na mafisadi na wahujumu uchumi

    (GMT+08:00) 2018-04-03 09:28:50

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan ametoa mwito wa kupambana na mafisadi, walanguzi na wahujumu uchumi wa nchi.

    Akilihutubia bunge la taifa Rais Al-Bashir amesema uchumi wa Sudan umekuwa unasumbuliwa na matatizo mengi tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kutokana na ulanguzi wa fedha, biashara ya magendo ya dhahabu na usambazaji wa bidhaa. Pia amesema kuna watu ndani ya mabenki wanaowasaidia.

    Amesisitiza kuwa serikali ya Sudan itaendelea na hatua kali kurejesha mali za taifa zilizoibiwa, na yeyote anayekutwa na hatia ya kufanya hivyo ni lazima aadhibiwe. Amesema mapambano dhidi ya ufisadi hayatasimamishwa hadi biashara ya magendo ya dhabahu, ulanguzi wa fedha, na ukiritumba wa bidhaa za kimsingi vitakapotokomezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako