• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Raia elfu 40 warejea Ghouta Mashariki nchini Syria

  (GMT+08:00) 2018-04-03 18:45:24

  Jumla ya raia elfu 40 wamerejea kwenye makazi yao katika eneo la Ghouta Mashariki, pembezoni mwa mji mkuu wa Syria, Damascus, ambapo jeshi la serikali linakaribia kuukomboa mji huo.

  Jeshi la Syria limekomboa miji yote ya Ghouta Mashariki isipokuwa wilaya ya mwisho inayoshikiliwa na waasi ya Douma, ambako hivi karibuni wapiganaji wa kiislamu wamekubali kuondoka.

  Mwezi uliopita raia 150,000 waliondoka Ghouta Mashariki wakati waasi walipoondolewa huko kutokana na mashambulizi mfululizo yaliyofanywa na jeshi la serikali ya Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako