• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:03:01

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo alasiri amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. Ri Yong Ho ambaye anapita Beijing.

    Pande hizo mbili zimekubaliana kutekeleza makubaliano ya viongozi wa nchi hizo mbili, kuimarisha ziara kati ya wakuu wa nchi hizo mbili na mawasiliano ya kidiplomasia katika sekta mbalimbali, kurithi na kuendeleza uhusiano wa kirafikiti kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Wang Yi amesema China itaendelea kuhimiza mazungumzo ya amani na kufanya juhudi ili kutimiza lengo la kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye penisula ya Korea na kujenga mfumo wa amani wa peninsula hiyo.

    Bw. Ri Yong Ho amesema Korea Kaskazini itafuata mwelekeo uliofafanuliwa na viongozi wa nchi hizo mbili katika mkutano uliofanyika hapa Beijing, na kufanya mawasiliano ya kimkakati na China kuhusu masuala ya peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako