• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Kampuni za chuma zalaumiwa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:21:43

    Kundi la Consumer Trust Citizens ambalo linatetea haki za raia limeitaka serikali kuchukua hatua za kuondoa chuma za hali duni ambazo zimefurika kwenye soko la Uganda.

    Kampuni tatu ambazo ni Pramukh Steel, Tembo Steels na Modern Steel, zinatuhumiwa kwa kuuza chuma ambazo hazijafikia ubora uliowekwa.

    Mwaka 2010 idara ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini humo ilifunga kwa muda kampuni ya Tembo Steels kwa kuzalisha chuma za hali duni.

    Idara hiyo inasema baadhi ya chuma za hali duni zinauzwa kwa bei rahisi hali ambayo inahatarisha usalama wa jumla wa ujenzi wa nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako