• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yasitisha uendelezaji wa maeneo ya Miji

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:23:52

    Serikali ya Tanzania imesitisha uendelezaji wa maeneo ya Mji wa Serikali na Chamwino na eneo linalozunguka maeneo hayo mkoani Dodoma.

    Katika maeneo hayo yaliyositishwa ujenzi kuna vijiji vya Msanga, Chahwa, Vikonje, Buigiri, Chamwino, Mahomanyika na Kikombo, kutokana na kufanyika ujenzi holela na mauziano ya ardhi yasiyo rasmi unaoendelea.

    Katika Tangazo lililotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi linasema kutokana na ufanyaji mapitio ya mpango kabambe wa Mji Mkuu wa Dodoma unaoendelea kuna umuhimu wa kusitisha shughuli za uendelezaji ardhi katika maeneo hayo.

    Alisema katika kutekeleza uhamishaji wa Mji Mkuu wa Serikali kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, serikali inafanya mpango kabambe wa Dodoma (2010), ili kuendana na mahitaji halisi ya uhamasishaji makao makuu una fursa nyingine za kiuchumi pamoja na mapitio ya mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako