• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yafuta makubaliano na Umoja wa Mataifa wa kuwapatia makazi mapya Waafrika wanaotafuta hifadhi

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:26:31

    Israel imefuta makubaliano iliyofikia na Umoja wa Mataifa ya kuwapatia makazi mapya Waafrika wanaotafuta hifadhi, ikiwa ni siku moja baada ya makubaliano hayo kutangazwa.

    Jumatatu mchana, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza kuwa makubaliano yamefikiwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Chini ya makubaliano hayo, mpango wa serikali wa kuwarejesha makwao watu wanaotafuta hifadhi kutoka Erotrea na Sudan ulifutwa, na badala yake, nusu ya wakimbizi watapelekwa nchi za Magharibi na wengine wataruhusiwa kuishi Israel.

    Hata hivyo, jana usiku, Bw. Netanyahu aliweka kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa anasitisha utekelezaji wa makubaliano hayo. Hatua hiyo imefikiwa baada ya kulaumiwa na baraza lake la mawaziri kwa kushindwa kujadiliana nao kabla ya kukubali mapendekezo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako