• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwindaji wasababisha dubu jike kutunza watoto wao kwa muda mrefu zaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-04 08:35:46

    Utafiti mpya unasema uwindaji umesababisha mabadiliko ya mwenendo wa dubu, hasa dubu jike wanaowatunza watoto wao.

    Kwa kawaida dubu jike wa kahawia wanaoishi kwenye peninsula ya Scandinavia wanaishi pamoja na watoto wao kwa mwaka mmoja na nusu, lakini siku hizi kwa wastani wanaishi pamoja na watoto kwa miaka miwili na nusu. Pengine watu wanafikiri dubu jike walibadilisha mienendo yao ili kuwalinda watoto wao wasiumizwe na wawindaji mpaka wawe wakubwa. Lakini hali halisi si kama watu wanavyofikiri, bali ni kwamba dubu jike wanaoishi peke yao wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufa kuliko wale wanaowatunza watoto.

    Dubu jike wanaowatunza watoto wanaoishi ni salama zaidi kwani wawindaji hawawaui. Watafiti wamesema kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2015, idadi ya dubu jike wanaowatunza watoto kwa miaka miwili na nusu imeongezeka kutoka asilimia 7 hadi asilimia 36.

    Watafiti wamesema mkakati huo mpya unaochukuliwa na dubu jike unafanya kazi za pande mbili, yaani dubu jike wanaweza kuishi kwa usalama zaidi na watoto wao, lakini pia wanazaliana kwa mara chache zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako