• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya usalama wa chakula ya Namibia yaridhisha kutoka na mavuno mazuri

    (GMT+08:00) 2018-04-04 09:46:09

    Ripoti ya idara ya tahadhari na habari kuhusu chakula ya Namibia (NEWFIU) imesema usalama wa chakula kwa kaya katika eneo kubwa la Namibia unaendelea kuridhisha, kutokana na msimu mzuri wa kilimo uliopita.

    Ripoti hiyo ilitolewa baada ya tathmini ya uzalishaji wa mazao kufanyika katika mikoa saba inayozalisha chakula kwa wingi, kati ya mwezi Februari na Machi mwaka huu.

    Wizara ya kilimo ya Namibia imesema lengo kuu la kazi hiyo lilikuwa ni kutathmini hali ya uzalishaji wa chakula kwenye mikoa inayozalisha chakula kwa wingi na kutoa ripoti ya tahadhari ya mapema kuhusu shughuli za uchumi zinazohusiana na madhara ya mafuriko, ukame, na matukio mengine muhimu.

    Idara hiyo pia imesema itaendelea kufuatilia hali na kutoa taarifa mpya kwa usahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako