• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yazindua kituo kipya cha kuzalisha umeme kwa nishati ya gesi

    (GMT+08:00) 2018-04-04 09:46:33

    Rais John Magufuli wa Tanzania amezindua kituo cha kuzalisha megawati 167.82 za umeme kwa nishati ya gesi mjini Dar es Salaam. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 344 ni sehemu ya juhudi za serikali ya Rais Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

    Mkurugenzi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Bw. Tito Mwinuka amesema megawati 167.82 zitaunganishwa kwenye gridi ya taifa.

    Waziri wa nishati wa Tanzania Bw. Medard Kalemani amesema mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji ulioko katika bonde la Stiegler utaanza kutekelezwa mwezi Julai, na kuwa bwawa kubwa kabisa kwenye Mto Rufiji na unatarajiwa kukamilika mwaka wa 2021. Ameongeza kuwa serikali itajenga miundombinu muhimu itakayosaidia utekelezaji wa mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako