• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatarajia jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti

  (GMT+08:00) 2018-04-04 17:53:52

  Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti na kuhimiza pande zote za nchi hiyo kuongeza nguvu kuendeleza uchumi wao na kuboresha maisha ya watu.

  Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Haiti, Bw. Wu amesema, anatarajia jumuiya ya kimataifa itaisaidia Haiti kuimarisha utulivu nchini humo na kutekeleza malengo ya maendelea endelevu ya mwaka 2030.

  Bw. Wu pia amesema, China imetoa mchango wake katika Mfuko wa Imani wa kukabaliana na Malaria ili kusaidia Haiti kukabiliana na mlipuko wa Malaria, na kuongeza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kushiriki kwenye hatua za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na mlipuko huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako