• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IGAD yaipongeza Kenya kwa kupitisha makubaliano ya biashara barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-04-04 18:26:49

  Shirika la Maendeleo la Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD limeipongeza Kenya kwa kuwa moja ya nchi za mwanzo kupitisha mfumo wa kuanzisha Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA), ambalo litakuwa soko moja kwa bidhaa na huduma katika bara hilo.

  Shirika hilo limesema, upitishwaji wa haraka wa muswada wa sheria wa kuanzisha Eneo hilo kunaonyesha nia thabiti ya kisiasa ya serikali ya Kenya katika kuimarisha mwingiliano wa Afrika kuhusu biashara kupitia kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kukuza soko moja huru katika bara hilo.

  Nchi zote za Afrika Mashariki, isipokuwa Burundi ambayo haikuhudhuria mkutano wa kilele Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi uliopita nchini Rwanda, zimesaini itifaki zote tatu zilizopitishwa katika mkutano huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako