• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Museveni aongeza ushuru wa TAXI

    (GMT+08:00) 2018-04-04 19:15:06

    Rais Yoweri Museveni ameongeza ushuru wa wahuduma wa Taxi kati kati mwa jiji la Kampala .

    Agizo hilo limetolewa kwa taxi zinazohudumu ndani ya kilomita 21 jijini Kampala.

    Wahudumu hao sasa watapaswa kulipa shililingi 720,000 kila mwaka .

    Ushuru huu mpya unajiri baada ya kikao cha halmashauri ya jiji ,wizara ya mambo ya ndani na wahudumu wa taxi wa Uganda.

    Mkurugenzi wa kitengo cha ushuru Fred Andema amesema wahudumu hao wanaingiza fedha za kutosha na hivyo lazima serikali ifaidike .

    Fedha hizo zitatumika kuboresha uchukuzi na kulipia wafanyikazi wa umma wa sekta hizo .

    Hata hivyo wahudumu hao wamesema wataongeza bei ya huduma za Taxi kwa wateja

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako