• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • PLO yasema watoto 350 wa Palestina wanashikiliwa na Israel

    (GMT+08:00) 2018-04-05 08:23:22

    Leo Aprili tano ni Siku ya watoto ya Palestina. Idara ya mambo ya wafungwa ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO imesema hivi sasa watoto wapatao 350 wa Palestina wanashikiliwa na Israel. Kwa mujibu wa idara hiyo, kati ya watoto hao, wasichana wanane na wavulana sita wanashikiliwa kwenye kituo cha kuwarekebisha vijana, na wengine wote wamefungwa kwenye magereza ya Israel, wengi wao wakiwa wanatoka Jerusalem mashariki. Idara hiyo pia imesema baadhi ya watoto waliteswa na kuhojiwa kikatili wakiwa kizuizini. Imefahamika kuwa mwaka 2015 Israel ilirekebisha vifungu vya sheria vinavyohusu muda wa vifungo dhidi ya watoto wa Palestina, na kuruhusu vifungo dhidi yao kufikia zaidi ya miaka kumi hadi maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako