Mkutano wa nne wa maofisa waandamizi wa ulinzi na usalama unaohusu kupambana na ujangili, umefanyika katika mbuga ya wanyama ya Kruger nchini Afrika Kusini.
Mkutano huo wa siku mbili ulihusu maswala ya kisheria na kutafuta njia zinazofanana za kuwaadhibu wale wanaokutwa na hatia za ujangili. Katika mkutano uliopita wa maofisa hao, ilifahamika kuwa nchi mbalimbali za SADC zina adhabu tofauti kwa makosa ya ujangili.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, nchi za SADC zimepitisha mkakati wa pamoja utakaohimiza juhudi za kupambana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori.
Katika miaka ya hivi karibuni eneo la SADC limeshuhudia ongezeko la biashara haramu ya wanyama na ujangili, hasa wa pembe za ndovu na faru.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |