• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa usalama wa kimataifa wafuatilia mfumo wa usalama wa kimataifa na mapambano dhidi ya ugaidi

  (GMT+08:00) 2018-04-05 19:37:42

  Mkutano wa 7 wa usalama wa kimataifa umefanyika jana mjini Moscow, Russia, ambapo wajumbe waliohudhuria mkutano huo walijadili mwelekeo wa kufanya juhudi katika kupambana na ugaidi katika siku zijazo na kusisitiza kulinda mfumo wa usalama wa kimataifa na maelewano, haki na usawa.

  Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Katibu wa mkutano wa usalama wa Russia Bw. Nikolai Patrushev amesema Umoja wa Mataifa ulitoa mchango mkubwa katika sekta ya kurekebisha na kushughulikia suala la uhusiano wa kimataifa. Lakini baadhi ya nchi zinajaribu kwenda kinyume na kanuni katika sekta ya usalama wa kimataifa, ambayo yanavunja utulivu wa hali duniani na kuizuia jumuiya ya kimataifa kukabiliana na changamoto na matishio ya usalama wa kimataifa.

  Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa taifa wa China Bw. Wei Fenghe amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kubadilishana maoni kuhusu usalama, kutatua mgogoro kwa amani, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usalama na ulinzi, kujenga mazingira ya usalama wa kimataifa yanayonufaishana na kugawana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako