• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais mpya wa Sierra Leone aapishwa

  (GMT+08:00) 2018-04-05 19:41:19

  Mgombea urais wa chama kubwa zaidi cha upinzani cha Sierra Leone cha SLPP, Bw. Julius Maada Bio ameapisha kuwa rais mpya jana usiku mjini Freetown mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu.

  Tume ya uchaguzi ya Sierra Leone jana imetangaza matokeo ya duru ya pili ya upigaji kura ambapo Bw. Bio amepata asilimia 51.8 ya kura na kumshinda mgombea kutoka chama tawala Bw. Samura Kamara aliyepata asilimia 48.19 ya kura.

  Habari zinasema, watu zaidi ya milioni 2.5 wa Sierra Leone wameshiriki kwenye upigaji kura huo ambapo kiwango cha upigaji kura kimefikia asilimia 81.11.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako