• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafungua shauri la mchakato wa kusuluhisha mgogoro wa kibiashara dhidi ya kifungu cha 232 cha Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-05 20:48:56

    Wizara ya Biashara ya China imesema, China leo imefungua shauri chini ya mfumo wa Shirika la Kimataifa la Biashara wa kusuluhisha mgogoro dhidi ya Marekani kuhusu kifungu cha 232 cha Marekani kinachoweka ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminium zinazoagizwa kutoka China.

    Ofisa wa idara ya sheria katika wizara ya biashara ya China amesema, kifungu hicho kimewekwa kwa sababu ya "kulinda usalama wa taifa", lakini ni hatua ya kujilinda kibiashara. Marekani kwa upande mmoja imechagua baadhi ya nchi na sehemu, kwa upande mwingine imeongeza ushuru kwa bidhaa kutoka baadhi ya nchi wanachama wa WTO ikiwemo China. Hatua hiyo imekwenda kinyume na kanuni ya kutokuwa na ubaguzi katika mfumo wa biashara kati ya pande nyingi, na ahadi yake ya kupunguza ushuru chini ya WTO na kanuni husika za uhakikisho, na imedhuru maslahi halali ya China ikiwa nchi mwanachama rasmi wa WTO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako