• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Russia akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:03:48

    Rais Vladimir Putin wa Russia jana amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi huko Ikulu ya Russia.

    Bw Wang amekabidhi salamu za pongezi za rais Xi Jinping wa China kwa Putin kutokana na kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia. Amesema China na Russia ni wenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote, na rais Xi anamkaribisha Rais Putin kufanya ziara nchini China mwezi Juni mwaka huu.

    Naye Rais Putin amesema anatarajia kudumisha mawasiliano ya karibu na rais Xi Jinping, na kutaka uhusiano kati ya nchi hizo mbili uweze kupata maendeleo zaidi.

    Bw Wang Yi pia amefanya mazungumzo na mwenzake wa Russia Bw Sergei Lavrov. Bw Wang amesema China itashirikiana na Russia katika kuhimiza mawasiliano na ushirikiano, na kulinda mfumo wa biashara huria ya dunia kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako