• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaanzisha mpango wa mafunzo ya kuhimiza sekta ya utalii kwa njia ya mtandao

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:04:10

    Bodi ya Utalii ya Kenya KTB imeanzisha mpango wa kitaifa wa kutoa mafunzo kwa mameneja wa bidhaa na mashirika ya utalii ili kuongeza uzoefu wa kuuza bidhaa za utalii kwenye mtandao wa internet.

    Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Utalii ya Kenya Bibi Betty Radier amesema bodi yake imeshirikiana na Kampuni ya Google, kampuni ya Safaricom, shirika la biashara la Kenya, Shirika la Huduma kwa wanyamapori nchini Kenya KWS, shirika la fedha la utalii, na ofisi ya mtandao wa KTB katika kutekeleza mpango huo wa mafunzo.

    Bibi Radier ametoa taarifa jijini Nairobi akisema Bodi ya Utalii ya Kenya itawafunza wafanyabiashara wa sekta ya utalii namna ya kuhimiza biashara kupitia mtandao wa internet. Ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhimiza matumizi ya usafiri wa ndani na kuhimiza sekta ya utalii ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako