• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa nchi tatu kuhusu ujenzi wa bwawa katika mto Nile waahirishwa licha ya kutopatikana muafaka

  (GMT+08:00) 2018-04-06 18:41:08

  Mkutano wa majadiliano wa nchi tatu zinazonufaika na maji ya mto Nile ambazo ni Sudan, Misri na Ethiopia umeahirishwa leo licha ya kutopatikana suluhisho juu ya mvutano uliopo kuhusu mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme nchini Ethiopia GERD.

  Akitangaza kufungwa kwa mkutano huo uliofanyika mjini Khartoum, waziri wa mambo ya nje ya Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amewaambia waandishi wa habari kuwa, nia ya kutafuta suluhu ya mvutano huo ilikuwepo lakini ilishindikana kutokana na tofauti za asili zilizopo kati nchi hizo.

  Bw. Ghandour amesema unahitajika muda mrefu zaidi wa kulijadili suala hilo, na kwamba sasa wanawaachia mawaziri wa umwagiliaji kutoka nchi hizo kujadili zaidi, na endapo watawahitaji watakuwa tayari kukutana tena.

  Mkutano huo ambao ulianza jana alhamisi iliyopita uliwajumuisha viongozi waandamizi kutoka nchi hizo tatu, mawaziri wa mambo ya nje, mawaziri wa maliasili ya maji na wakuu mbalimbali wa vyombo vya usalama vya nchi hizo ambao wote kwa pamoja walitaka kuondoa tofauti zilizopo kuhusu ujenziwa bwawa hilo.

  Mkutano huo ulifanyika ikiwa ni baada ya wakuu wa nchi hizo tatu kukutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia mwezi Januari mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako