• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali

  (GMT+08:00) 2018-04-06 18:53:21

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alifafanua kuwa vitendo vya kujilinda kibiashara si njia sahihi ya kutatua mivutano ya biashara, na pia alieleza kuunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali.

  Vita vya kibiashara vina athari mbaya kwa pande husika na zinaathiri maendeleo ya uchumi wa biashara. Kufanya mazungumzo ni njia sahihi ya kutatua suala. Suala la ulimwengu linapaswa kutatuliwa kwa mpango wa ulimwengu ambao unahitaji kutekelezwa chini ya msingi wa pande mbalimbali. Mfumo wa biashara wa pande mbalimbali ambao kiini chake ni shirika la biashara la kimataifa WTO siku zote ulifanya umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya biashara ya kimataifa. Kuanzisha vita ya biashara si njia ya kutatua mgogoro wa biashara, lakini kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ndiyo njia sahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako