• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Rwanda nchini China asema "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umetoa uhai kwa mawasiliano na maendeleo yenye uratibu ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-04-08 15:47:10

    Balozi wa Rwanda nchini China Charles Kayonga amesema kuhimizwa kwa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kumeimarisha msingi imara kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kutoa nguvu ya uhai kwa ajili ya mawasiliano na maendeleo yenye uratibu katika bara la Afrika.

    Akizungumza kwenye hafla ya kumbukumbu ya miaka 24 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda iliyofanyika kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini China, balozi Kayonga amesema miaka 24 iliyopita, mauaji hayo yaliishangaza dunia nzima, na sasa Rwanda ina utulivu wa kisiasa, ustawi wa kiuchumi na umoja wa kikabila, na inashukuru China kutokana na juhudi zake za kuisaidia kudumisha amani na utulivu. Amesema China siku zote ni rafiki wa kweli wa Rwanda, na Rwanda inapenda kushirikiana na China kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja iliyo ya kuheshimiana na kutafuta maendeleo ya pamoja kwa kupitia ushirikiano. Anasema,

    "katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, China imetoa mchango mkubwa kwa nchi za Afrika kuweza kujitegemea kiuchumi na kupata maendeleo endelevu, huku ikisaidia kuhimiza maendeleo ya viwanda barani Afrika na kuinua uwezo wa kuuza nje bidhaa zinazotengenezwa barani Afrika, vilevile China imetuingizia rasilimali nyingi. Kwa hiyo naona 'jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja' inamaanisha kusaidiana, kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja."

    Balozi Kayonga amesema Rwanda iko katika eneo la "katikati" barani Afrika, na kuna nguvu kubwa kwenye uchukuzi barabarani na kufanya kazi ya kuwa kiunganishi kwenye mchakato wa mafungamano barani Afrika. Amesema China ikiwa ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika na nchi inayowekeza zaidi barani humo, imekuwa ikijitahidi kushirikiana na Afrika kutafuta sekta mpya zinazoweza kuleta ongezeko kwenye ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji. Chini ya mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ujenzi wa mtandao wa reli wa Afrika Mashariki na mchakato wa mawasiliano ya Afrika vimehimizwa kwa kasi na kutoa fursa mpya kwa nchi mbalimbali za Afrika kupata maendeleo kwa pamoja. Anasema,

    "Mpango uliotolewa na China wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja" unajumuisha nchi mbalimbali duniani. Mtandao wa reli wa Afrika ni mfano mzuri, kutoka mashariki hadi magharibi, kutoka kaskazini hadi kusini, umeongeza kasi ya mchakato wa maendeleo ya kiviwanda ya nchi mbalimbali na kuhimiza maendeleo yao ya kiuchumi. Mpango wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' umeiletea Afrika faida kubwa, na hatua 10 za ushirikiano kati ya China na Afrika pia zinatekelezwa, hayo yote yamechangia ukuaji wa uchumi wa Afrika na kuinua nguvu etu ya ushindani."

    Balozi Kayonga anasema ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pia umehimiza mawasiliano na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Afrika, na kufanya biashara huria kuwa ni sauti ya pamoja ya nchi mbalimbali za Afrika. Tarehe 21, Machi, nchi 44 za Afrika zilisaini makubaliano ya eneo la biashara huria la Afrika mjini Kigali, Rwanda, hatua ambayo sio tu itahimiza biashara kati ya nchi hizo, bali pia kuongeza mawasiliano kati ya nchi za Afrika na wenzi wengine wa kibiashara. Anasema,

    "Naona viongozi wa nchi za Afrika waliosaini makubaliano ya eneo la biashara huria la Afrika wana busara, na kupitia msukumo wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na eneo la biashara huria la Afrika, mafungamano barani Afrika yataendelezwa hadi kuwa mafungamano ya kiuchumi. Kutokana na uungaji mkono mkubwa wa China, kupitia muundo huo, sisi hatutakuwa na vizuizi vya kibiashara na biashara itakuwa rahisi na nzuri zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako