• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani hakika itashindwa kwenye vita ya kibiashara inayotaka kufanya na China kutokana na makosa yake matatu

  (GMT+08:00) 2018-04-08 19:23:41

  Historia huwa haijirudii, lakini huweza kueleza. Wakati serikali ya Trump inapotishia China kwa fimbo la mgogoro wa kibiashara, watu wanaweza kukumbuka kauli maarufu aliyoitoa Jenerali Omar Bradley tarehe 15, Mei mwaka 1951 bungeni akiwa mwenyekiti wa wanadhimu wakuu kwa wazo la kutaka kupanua Vita ya Korea hadi China. Kauli hiyo ni kuwa "itakuwa ni vita isiyofaa, katika sehemu isiyofaa, katika wakati usiofaa na dhidi ya adui asiyefaa" Hivi sasa, serikali ya Trump inataka kuanzisha vita ya biashara na China, jambo ambalo pia amefanya makosa matatu na hakika Marekani itashindwa katika vita hiyo.

  Kwanza ni mawazo yenye makosa: mtazamo ilio nao serikali ya Marekani bado ni wa vita baridi, kutoka kuichukulia China kuwa ni "adui wa ushindani" kwenye ripoti ya mkakati wa usalama wa taifa iliyotolewa baada ya Trump kuingia madarakani, hadi kutangaza "mkakati wa India na Pasifiki" alipofanya ziara yake ya kwanza katika Asia Mashariki na kusaini Sheria ya Usafiri wa Taiwan. Serikali ya Marekani inaona ukuaji wa China utaipa changamoto hadhi ya uongozi wa Marekani duniani hivyo kutumia kila iwezalo kukwamisha maendeleo ya China. Hatua hizo zimeonesha kuwa Marekani haina imani na hofu na kurudi nyuma kwao na kuongezeka kwa nguvu za jumla za taifa la China.

  Pili ni adui wa makosa: Marekani inaweza kutafuta maslahi kwenye nchi za Umoja wa Ulaya, Japan na Shirikisho la Urusi, lakini ikiwa nchi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi, China haitaruhusiwa kulengwa. Baada ya kutangaza kuongoza ushuru wa dola za kimarekani bilioni 50 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China na kutangaza kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100, China hairudi nyuma, na imetangaza kutumia nguvu zinazofanana na kuongeza ushuru wenye thamani zinazofanana dhidi ya bidhaa za Marekani.

  Tatu ni njia zenye makosa: Trump alikuwa mfanyabiashara na ana imani na "usanii wake wa biashara". Safari hii, Marekani inataka kutumia njia ya kuanzisha vita ya biashara na China kuhimiza mazungumzo, na kuihadaa China. Wakati huohuo, inatoa tishio na kuimarisha hatua za uchochezi ili kuilazimisha China kusalimu amri. Lakini China siku zote inafuata utamaduni wake kuwa "utajiri na heshima haviwezi kumhonga yeye, wala matishio na nguvu vinaweza kumfanya asalimu amri." zamani China haikuwa na pesa haikusalimu amri, sasa China imeendelea na inaweza kukabili vitendo vyovyote vya uchochezi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako