• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda na WHO wamesema wataanzisha kituo cha utenganishaji kupambana na kipindupindu

    (GMT+08:00) 2018-04-09 08:48:21

    Mamlaka za afya kwenye wilaya ya Kagadi iliyoko kati magharibi mwa Uganda, na Shirika la afya duniani WHO, wameanzisha kituo cha utenganishaji ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipundupindu. Ofisa wa afya wa wilaya ya Kagadi Bw James Owolo, amesema kituo hicho kinaweza kupokea wagonjwa zaidi 100.

    Homa ya kipindupindu imelipuka katika wilaya ya Hoima, ambako wakimbizi 40 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

    Chama cha msalaba mwekundu nchini Uganda kimesema ujio wa wakimbizi kutoka DRC umefanya idara za afya nchini humo kuzidiwa uwezo na kuwalazimu wakimbizi hao kuishi kwenye maeneo machafu. Hali hiyo imechochea kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu tangu mwezi Februari. Inakadiriwa kuwa wakimbizi zaidi ya elfu 70 kutoka DRC wameingia nchini Uganda tangu mwezi Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako