• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-04-09 09:00:34

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana hapa Beijing alikutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Li Keqiang amesema uchumi wa dunia umedumisha mwelekeo wa kufufuka, lakini msingi wake si imara. Vilevile, vitendo vya upande mmoja na vya kujilinda kibiashara vimeibuka, na hali zisozotabirika kwenye mazingira ya kimataifa bado zimejitokeza. Amesema China imefungamana na dunia kwa kina, na inahitaji mazingira ya nje yenye amani na utulivu. China ikiwa nchi kubwa inayoendelea, inapenda kubeba majukumu ya kimataifa yanayolingana na uwezo wake, na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuunga mkono mafungamano ya dunia. Bw. Li pia amepongeza ushirikiano na uhusiano uliopo kati ya China na Umoja wa Mataifa.

    Kwa upande wake Bw. Guterres amesema China ni nguzo muhimu ya amani na ushirikiano wa kimataifa, na Umoja wa Mataifa unapenda kuzidisha ushirikiano na China katika pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako