• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Jumuiya ya Madola: Cheptegei wa Uganda ashinda dhahabu kwenye mbio za mita 5000

    (GMT+08:00) 2018-04-09 10:51:29

    Mwanariadha Joshua Cheptegei ameshinda medali ya dhahabu baada ya kuibuka namba moja kwenye mbio za mita 5000 kwenye mashindano ya jumuiya ya madola yanayoendelea nchini Australia.

    Hii ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi za Afrika mashariki katika michezo hiyo msimu huu tangu ianze April 4.

    Akizungumza na waandishi wa habari Cheptegei amesema ilimlazimu kuyazoea mazingira ya majira ya mwanzo wa mwaka kwani yeye amezoea zaidi kushiriki kuanzia mwezi Agosti na kuendelea, hivyo ilimbidi afanye mazoezi sana.

    Hii ni medali ya dhahabu ya 14 kati ya medali 50 ilizojikusanyia Uganda tangu ianze kushiriki michezo hiyo.

    Kwa Cheptegei anatarajiwa pia kushiriki mbio za mita 10,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako