• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kwanza la watu la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) lafunguliwa

    (GMT+08:00) 2018-04-09 16:52:34

    Kongamano la kwanza la watu la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) leo limefunguliwa huko Xian, mkoani Shaanxi nchini China, na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 80 kutoka nchi 12.

    Kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Wajibu wa mashirika ya kiraiaļ¼š Kuhimiza amani na ushirikiano wa kikanda, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja". Wajumbe hao wakiwemo maofisa wa zamani wa serikali, wale kutoka mashirika na kiraia na jopo la washauri bingwa wamejadili namna ya kufanya mashirika ya kiraia kutoa nguvu ili kuhimiza utulivu, ustawi na maendeleo ya kikanda.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano hilo, naibu spika wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China Bw. Ji Bingxuan amesema, kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kutimiza maendeleo ya pamoja, ni sauti na pendekezo la China, pia ni juhudi zinazofanywa kwa pamoja na serikali ya China na wananchi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako