• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alibaba yatoa nafasi zaidi ya milioni 36.8 za ajira kwa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-04-09 16:56:15

    Kampuni ya biashara kupitia mtandao wa internet ya China Alibaba ilitoa nafasi za ajira zaidi ya milioni 36.8 kwa mwaka jana kutokana na mfumo wake wa manunuzi ya rejareja kupitia mtandao.

    Ripoti iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Renmin cha China imeonyesha kuwa, majukwaa mbalimbali ya kampuni hayo kama Tmall na Taobao, ambayo yana zaidi ya watumiani milioni 500, yalitoa nafasi milioni 14.05 za ajira kwa wauzaji kupitia mtandao wa internet kwa mwaka jana. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, nguo, vitambaa, na bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani ziliongoza kwa bidhaa zilizotoa nafasi kubwa zaidi ya ajira.

    Katika robo ya nne ya mwaka jana, kampuni ya Alibaba ilishuhudia ongezeko la mapato la asilimia 56 ikilinganishwa na mwaka juzi kipindi kama hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako