• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yapiga marufuku uuzaji wa makaa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-04-09 18:26:48

    Serikali ya Uganda imepiga marufuku uuzaji wa makaa kwenda Kenya katika juhudi za kulinda misitu nchini humo.

    Kamishena wa wilaya ya Busia Uganda, Hussein Kato Matanda, ametangaza kwenye eneo la mpakani kwamba sasa uuzaji wa makaa ni kinyume cha sheria.

    Awali Kenya imeweka marufuku ya ukataji miti na uuzaji wa makaa baada ya kubaini kuwa misitu mingi imeangamia kutokana na shughuli hizo.

    Kutokana na marufuku ya Kenya wadau wa makaa nchini Uganda wamekuwa na soko zuri, huku gunia moja likapanda bei maradufu hadi dola 22 kutoka bei ya awali ya dola 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako