• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Israel lafanya mashambuzi ya anga dhidi ya kundi la Hamas ukanda wa Gaza

    (GMT+08:00) 2018-04-10 09:25:12

    Jeshi la Israel limetoa taarifa likisema jana lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kituo kimoja cha kundi la Hamas kilichoko kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

    Taarifa imesema jeshi la anga lilifanya shambulizi hilo kujibu kitendo cha wapalestina watatu kujipenyeza nchini Israel na kutega mabomu mawili ya kienyeji kwenye eneo la mpaka kati ya Israel na ukanda wa Gaza.

    Jeshi la Israel lilisema limefuatilia kwa karibu vitendo vya hujuma vilivyopangwa na kufanywa na kundi la Hamas, na kusisitiza kuwa haliruhusu eneo la mpaka kati ya Israel na Gaza liangukie kuwa eneo la vita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako