• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mpya wa Botswana aahidi kuhimiza ushirikiano na Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-04-10 09:33:23

    Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana amefanya ziara ya siku moja nchini Zimbabwe, na kueleza matumaini ya kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Baada ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake rais Emmerson Mnangagwa, Rais Masisi amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaimarishwa, na anatarajia kuwa rais Mnangagwa,atafanya ziara nchini Botswana kwa mara nyingine tena katika nusu ya pili ya mwaka huu.

    Rais Masisi amesema akiwa ni rais mpya wa Botswana, ziara yake hii inalenga kujitambulisha kwa viongozi wa nchi jirani na kuonesha uungaji mkono wake, na kuhimiza mawasiliano kati ya nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako