• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Kenya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-04-10 09:33:56

    Sudan na Kenya zimeeleza nia ya kuimarisha uhusiano kati yao hususan katika sekta ya uchumi.

    Taarifa hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo kati ya makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Bw. Hassan Saleh na naibu wa rais wa Kenya Bw. William Ruto.

    Bw. Saleh amesema nchi hizo mbili zimesisitiza kuwa ziko tayari kushirikiana kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara, hasa baada ya kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Sudan.

    Bw. William Ruto alieleza ahadi ya Kenya ya kutafuta amani na utulivu katika sehemu ya Pembe ya Afrika. Pia amesema Kenya inajiandaa kutoa mchango zaidi katika kutimiza amani nchini Somalia, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako