• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hoteli ya kwanza ya anga ya juu kufunguliwa mwaka 2022

  (GMT+08:00) 2018-04-10 09:54:23

  Kampuni ya Orion Span ya Marekani imetangaza kujenga hoteli ya kwanza ya anga ya juu. Hoteli hii itafunguliwa mwaka 2022 na gharama ya kukaa katika hoteli hii kwa siku 12 ni dola za kimarekani milioni 9.5.

  Kampuni hiyo imesema inapanga kurusha hoteli ya anga ya juu iitwayo "stesheni ya Aurora" mwaka 2021. Hoteli hii itakuwa na vitengo kadhaa ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita 13 na upana wa mita 4, ukubwa wa vyumba vya hoteli hii utakuwa karibu sawa na ukubwa wa ndege aina ya Gulfstream G550, na hoteli hii itaweza kupokea watalii wanne na wafanyakazi wawili kwa wakati mmoja.

  Hoteli hii itasafiri kwenye mzingo ulioko kilomita 320 juu ya dunia, itazunguka dunia kwa mzingo mmoja kila baada ya dakika 90.

  Mpango huo bado uko kwenye kipindi cha kukusanya uwekezaji, lakini sasa watu wanaweza kuweka nafasi safari ya kwenda hoteli hii kwa kulipa dola za kimarekani elfu 80 kama amana ya kwanza.

  Habari zinasema kwenye hoteli hii watalii watapata kuishi kama wanaanga, kuhisi ukosefu wa nguvu za mvutano wa dunia, kupiga picha ya dunia, kufanya majaribio ya kisayansi, kupanda mboga, kutazama mwanga aina ya aurora, na kutazama macheo na machweo kwa zaidi ya mara 10 ndani ya siku moja. Lakini kabla ya kwenda hoteli hii, watalii wanahitaji kupata mafunzo kwa miezi mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako