• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Kenya: Baada ya kukosa medali ya dhahabu kwenye riadha mitaa 10000 wanawake kuwekeza nguvu katika matukio mingine ya leo

    (GMT+08:00) 2018-04-10 10:18:19

    Baada ya kukosa medali za dhahabu katika baadhi ya matukio ya riadha ambayo ilikwekeza nguvu nyingi, Timu ya Kenya inayoshiriki michezo ya jumuiya ya madola nchini Australia, imeendelea na mikakati ya kuhakikisha inapata medali hizo kupitia matukio mengine yakiwemo ya leo.

    Leo kuna matukio takribani saba amabyo Kenya itashiriki, yakiwemo riadha, mchezo wa vishada, tennis ya meza, mashindano ya baiskeli, na kuogelea.

    Kwa upande wa riadha, Kenya leo itawakilishwa na wakimbiaji wawili wanawake kwenye mita 1500 walioingia fainali ambao ni Mary Wangari na Beatrice Chepkoech.

    Kiongozi wa timu ya Kenya, Barnabas Korir amesema jambo lililopo sasa ni kuangalia zaidi michezo na matukio yaliyobaki kwani nafasi bado ipo ya kukusanya medali zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako