• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu ya Zanzibar: Miamba sita hatarini kushuka Ligi Kuu Pemba

    (GMT+08:00) 2018-04-10 10:18:41

    WAKATI Ligi Kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba ikielekea ukingoni, timu sita zipo kwenye hatari ya kushuka daraja msimu ujao.

    Miamba hiyo ni pamoja na Okapi, Chuo Basra, Young Islander, Dogomoro, FSC na Kizimbani na baadhi ya timu hizo zimebakiwa na michezo mitatu na nyingine miwili.

    Hata hivyo, ligi hiyo imefikia patamu kwa timu zilizoko katika nafasi ya kuwemo kwenye nne bora ambazo hatimaye zitacheza hatua ya nane bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar.

    Vigogo hivyo ni Mwenge inayoongoza msimamo kwa kuwa na pointi 47, ikifuatiwa na Opec yenye 43, Hard Rock 40, na Jamhuri 38, na zingine zikiwa ni Shaba, Chipukizi, New Star na Wawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako