Kwenye mkutano wa mwaka wa baraza la Asia la Bo'ao, rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba akisema katika miaka 40 iliyopita, China imefanikiwa kufungua mlango katika pande zote, kujiunga na Shirika la Biashara Duniani WTO, kutoa mapendekezo ya kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kutoa mchango katika kukabiliana na msukosuko wa fedha wa Asia na dunia, kuchangia asilimia 30 katika ongezeko la uchumi wa dunia, kuwa nguvu muhimu ya kutuliza na kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia, na kusukuma mbele amani na maendeleo ya binadamu. Mageuzi na ufunguaji mlango ni mapinduzi ya pili ya China, vimekidhi mahitaji ya watu kuhusu maendeleo, uvumbuzi na maisha bora, pia vimeendana na mahitaji ya watu wa nchi mbalimbali kuhusu maendeleo, ushirikiano na maisha yenye amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |