• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa wito wa kujenga kwa pamoja Asia na dunia yenye amani, utulivu, ustawi na uwazi

    (GMT+08:00) 2018-04-10 11:14:13

    Akihutubia Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao, rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa nchi mbalimbali kuheshimana, kutendeana kwa usawa, kutofanya umwamba, kutojinufaisha kwa kuhujumu maslahi ya nchi nyingine, na kudhibiti migogoro ya kimataifa kwa hatua mwafaka. Pia amezitaka nchi mbalimbali zitekeleze wajibu wa kimataifa na kulinda kithabiti utaratibu na mfumo wa kimataifa wenye katiba ya Umoja wa mataifa kuwa kiini chake, ili kutimiza usalama wa pamoja.

    Kwa upande wa uchumi, rais Xi amependekeza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kushirikiana kwa njia ya kunufaishana katika kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, kuhimiza mafungamano ya kibiashara na kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.

    Rais Xi ametoa wito kwa nchi zenye staarabu tofauti kufundishana na kushirikiana katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ili kuzijenga Asia na dunia nzima ziwe na amani, utulivu, ustawi na uwazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako