• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asema China italegeza zaidi udhibiti wa kuingia sokoni mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-04-10 11:31:58

    Akihutubia Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao, rais Xi Jinping wa China amesema mwaka huu China italegeza kwa kiasi kikubwa udhibiti wa kuingia kwenye soko la China.

    Amesema hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na kuhakikisha sera iliyotolewa mwaka jana ya kulegeza udhibiti wa uwekezaji wa kigeni kwenye sekta za benki, hisa na bima inatekelezwa kihalisi, kupunguza vizuizi kwa mashirika ya kifedha ya nchi za nje na kupanua ushirikiano wa kifedha kati ya China na nchi za nje.

    Amesema kwenye sekta ya utengenezaji bidhaa, China itapanua wigo wa uwekezaji wa nje hasa kwenye sekta ya magari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako