• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono uchunguzi kuhusu tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-10 17:59:57

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Wu Haitao amesema, China inaunga mkono uchunguzi dhidi ya tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali wilayani Douma, nchini Syria.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana, balozi Wu amesema China inaunga mkono uchunguzi huo ili matokeo yenye msingi wa ushahidi kamili na yanayoweza kustahimili majaribu ya kihistoria na ukweli halisi yanaweza kufikiwa, ili watuhumiwa na watu wanaohusika waweze kufikishwa mbele ya sheria. Amesema China ina wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za shambulizi la silaha za kemikali lililotokea hivi karibuni nchini Syria na wahanga wa shambulizi hilo.

    Balozi Wu ameongeza kuwa daima China inapinga matumizi ya nguvu au vitisho katika masuala ya kimataifa, na daima inapendelea kushikilia Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako