• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aeleza hatua za nchi hiyo katika kufungua mlango zaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-10 19:03:34

    Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la Asia la Boao. Katika hotuba hiyo, rais Xi ameeleza hatua muhimu za kuzidisha ufunguaji mlango wa China kwa nje, na kusema hiyo sio tu ni hatua muhimu za China kuzidi kufungua mlango kwa duru mpya katika zama mpya, bali pia inafungua "Mlango wa Fursa ya China" kwa ufufukaji wa uchumi wa dunia.

    Hotuba ya rais Xi imetoa sauti imara ya kuzidisha mageuzi na ufunguaji wa mlango. "Mageuzi na Ufunguaji wa Mlango" ni neno muhimu la mkutano huo wa Boao. Huu ni mwaka wa 40 tangu China itekeleze sera ya "Mageuzi na Ufunguaji wa Mlango", rais Xi amekumbusha mafanikio yaliyopatikana nchini China katika miaka 40 iliyopita, ambayo yamethibitsha kuwa sera hiyo ni hatua inayoamua hatma ya China na kutatua suala gumu la ongezeko la uchumi na maendeleo ya dunia. Rais Xi ameahidi kuwa China itaendelea kuwa mjenzi wa amani wa dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa.

    Vilevile rais Xi ametangaza hatua mpya za ufunguaji mlango na kuwakaribisha nchi nyingine kujinufaika na maendeleo ya China. Kwenye hotuba yake, rais Xi ametangaza hatua nne muhimu, ambazo ni pamoja na kulegeza kwa kiasi kikubwa udhibiti wa kuingia kwenye soko la China, kujenga mazingira ya uwekezaji yenye mvuto zaidi, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu na kuongeza uingizaji wa bidhaa kutoka nje. Hatua hizo mpya sio tu zitaharakisha kuihimiza China kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa, bali pia zitaleta fursa kubwa na nafasi za maendeleo kwa maendeleo ya nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako