• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafurahi kuona Marekani ikitoa ishara chanya

    (GMT+08:00) 2018-04-11 18:54:53

    Rais Xi Jinping wa China jana alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa baraza la Asia la Boao, ambayo imeeleza hatua na sera muhimu za kuzidisha mageuzi na ufunguaji wa mlango. Hotuba hiyo imepongezwa na jumuiya ya kimataifa na rais Donald Trump wa Marekani pia ametoa jibu chanya juu ya hotuba hiyo.

    Makala iliyotolewa na mchambuzi wa Kituo cha Televisheni cha China CCTV imesema, China itaendelea kuhimiza ufunguaji wa mlango kwa kufuata mpango uliowekwa. Katika miaka 40 iliyopita, watu wa China wameshikilia sera ya msingi ya ufunguaji mlango na kufanikiwa kutimiza mabadiliko ya kufungua kwa pande zote. China imekuwa nguvu ya kutuliza na kuimarisha ongezeko la uchumi wa dunia, na kutoa mchango katika amani na maendeleo ya binadamu.

    Pia makali hiyo imesema, Gavana wa Benki Kuu ya China Bw. Yi Gang ametangaza hatua halisi na ratiba za kupanua ufunguaji wa mlango katika sekta ya fedha, ambayo imethibitisha kuwa China siku zote inatimiza ahadi yake. Kama Marekani ikitaka kufanya vita ya kibiashara, itapoteza fursa ya kuzidi kufanya ushirikiano na China na fursa ya kujinufaika na maendeleo ya China.

    Aidha, mchambuzi huyo ameongeza kuwa ni vema kuona Marekani inatoa ishara chanya, lakini bado inapaswa kuangalia maneno na vitendo vyake, haswa kuangalia hatua yake inayofuata. Amesema Marekani inapaswa kufahamu hali ya jumla, na kwamba kutoa matakwa yasiyo na msingi na kuchukua hatua za upande mmoja hakutapokelewa. Hivi sasa maendeleo ya pamoja ni mwelekeo wa dunia, na yanahitaji msingi wa mfumo wa biashara wa pande nyingi na kupinga kujilinda kibiashara kwa upande mmoja. Pande hizo mbili zinatakiwa kushikilia kanuni za kunufaishana ili kupata mafanikio ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako