• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asema daima China haitasitisha mageuzi yake

    (GMT+08:00) 2018-04-11 20:26:14

    Leo asubuhi, rais Xi Jinping wa China amekutana na wakurugenzi wa sasa na wajao wa Baraza la Asia la Boao, na kuzungumza na wajasiriamali wa ndani na nje ya China wanaohudhuria mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza hilo huko Boao, mkoani Hainan.

    Akizungumza na wasimamizi wa makampuni mbalimbali ikiwemo CP ya Thailand, shirikisho la wafanyabiashara la Marekani, kampuni ya magari ya Japan Toyota na kampuni ya bima ya Uingereza Prudential, rais Xi anasema daima mageuzi ya China hayatasita na mlango wa China kwa nje hautafungulwa. Amesema China itashikilia kuendeleza uchumi ulio wazi wa dunia, na kutoa mchango kwa maendeleo ya Asia na Dunia. Ameongeza kuwa China inazikaribisha pande mbalimbali kunufaika na matunda ya mageuzi, ufunguaji mlango na maendeleo ya China. Anasema,

    "Mwaka jana, China ilifanya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Mwezi Machi mwaka huu, ilifanya mikutano miwili. Kama nilivyozungumza katika mkutano wa jana, shughuli hizo zimetoa ishara kuwa China itapiga hatua zaidi kutekeleza mageuzi na ufunguaji mlango, kufanya mfumo wa China upevuke zaidi, kufanya maendeleo kuwa na ubora zaidi, kufanya usimamizi kuwa na ufanisi zaidi, na cha muhimu ni kuwafanya watu wawe na hisia ya kupata, kufurahi na usalama."

    Rais Xi amesema China itatoa mazingira bora ya kibiashara kwa makampuni ya ndani ya nje ya China, na kuwa na matumaini kuwa yanaweza kupata mafanikio zaidi katika mchakato huo. Amesisitiza kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linalenga kufanya mageuzi ya China kunufaisha binadamu na kutimiza mafanikio na maendeleo ya pamoja.

    Wajasiriamali hao waliohudhuria mkutano huo na rais Xi, wamesema wanapenda kutumia vizuri fursa zilizopo, kushiriki kwenye mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China na "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kufanya makampuni yao yapate maendeleo zaidi na kuleta ustawi zaidi kwa uchumi wa Asia na wa dunia.

    Huu ni mwaka wa kubadilisha awamu kwa bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Asia la Boao, na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon atakuwa mwenyekiti wa awamu mpya ya bodi hiyo. Akizungumza na wakurugenzi wa sasa na wajao wa Baraza la Asia la Boao, rais Xi anasema,

    "Katika miaka mingi iliyopita, mwenyekiti Bw Yasuo Fukuda, naibu mwenyekiti Bw Zeng Peiyan na wakurugenzi mbalimbali mmetoa maoni na mapendekezo yenye maana juu ya masuala makubwa yanayohusu maendeleo ya Asia na uchumi wa dunia, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya Baraza la Asia la Boao. Nina matumaini kuwa chini ya uongozi wa mwenyekiti Ban Ki-moon na naibu mwenyekiti Bw. Zhou Xiaochuan, awamu mpya ya bodi ya wakurugenzi ya Baraza hilo italeta maendeleo zaidi kwa kazi mbalimbali, ili kuchangia zaidi amani na maendeleo ya Asia na dunia."

    Mwenyekiti wa sasa wa bodi ya wakurugenzi Bw Yasuo Fukuda na mwenyekiti mteule Bw. Ban Ki-moon wametoa hotuba wakisema hotuba aliyotoa rais Xi Jinping katika mkutano wa jana ina maana kubwa wakati utandawazi na sera ya pande nyingi vinakabiliwa na changamoto. Wamesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kujifunza kutoka kwa China na kufuata njia ya maendeleo kwa mageuzi, ufunguaji mlango na ubunifu, badala ya kujifungia, kujilinda na kufuata sera ya upande mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako