• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya jumuiya ya madola: Kenya yaangushwa na Jamaica, wanamichezo 8 yadaiwa kutoroka

  (GMT+08:00) 2018-04-12 08:28:37
  Kenya imekosa medali ya dhahabu katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa upande wa wanawake, katika michezo ya jumuiya ya madola inayoendelea nchini Australia, baada ya Mjamaica Aisha Praught kumaliza wa kwanza kwa muda wa dakika 9 na sekunde 21.

  Matumaini ya kunyakua medali ya dhahabu sasda yamehamia leo wakati mbio za mita 800 kwa upande wa wanaume.

  Wakati huo huo, Wanariadha wanane wa Cameroon hawaonekani katika makaazi yao katika michezo ya Jumuiya madola nchini Australia, maafisa wa timu hiyo wametaarifu.

  Afisa wa habari Simon Molombe amesema maafisa wanachukulia kama wanariadha hao wametoroka na kwamba wameripotiwa kwa maafisa wa polisi nchini humo.

  Wanyanyua vyuma vya uzito watatu na mabondia watano walionekana mara ya mwisho katika muda tofuati Jumatatu na Jumanne, alisema.

  Cameroon imesema kundi la wanariadha hao wana viza halali za kudumu hadi Mei 15.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako