• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wasema utaendelea kuhamasisha upatikanaji wa fedha za mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya huwa

    (GMT+08:00) 2018-04-12 08:42:54

    Umoja wa Afrika umesema utazisaidia serikali za nchi za Afrika kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kupitia michango ya ndani ya taifa (NDC).

    Kamishna wa maendeleo ya vijijini na kilimo wa Umoja wa Afrika Bibi Josefa Sacko, amesema Umoja wa Afrika utahakikisha unazisaidia serikali za nchi za Afrika kufanikisha malengo yake. Amesema mafanikio kwenye kutimiza malengo ya ukusanyaji wa fedha zinahusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, yataamua kasi ya nchi za Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa baada ya mwaka 2020.

    Bibi Sacko amezitaka serikali za nchi za Afrika kuharakisha mijadala na wadau wa kimataifa ili kutafuta uungaji mkono wa kifedha na kiufundi. Amekumbusha kuwa serikali zinatakiwa kuwashirikisha wasomi na watu wa sekta binafsi kwenye mchakato wa kukusanya fedha hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako