• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yatarajia kupata pato la dola bilioni 1 kila mwaka kutokana na gesi asilia iliyogunduliwa na kampuni ya China

    (GMT+08:00) 2018-04-12 09:40:27

    Serikali ya Ethiopia inatarajia kupata pato la dola bilioni 1 za kimarekani kila mwaka kutokana na gesi asilia iliyogunduliwa hivi karibuni.

    Gesi asilia yenye akiba ya futi za ujazo bilioni 7 hadi 8 imegunduliwa hivi karibuni na kampuni ya Poly-GCL ya China nchini Ethiopia.

    Waziri wa madini, gesi na petroli wa Ethiopia Bw. Motuma Mekassa amesema, Ethiopia inatarajia kupata dola bilioni moja za kimarekani kwa kuuza gesi katika mwaka wa kwanza, na pato hilo linaweza kuongezeka katika miaka ifuatayo kutokana na akiba kubwa ya gesi.

    Bw. Mekassa amesema kampuni hiyo ya China pia inatarajiwa kujenga kiwanda cha kusindika gesi asilia katika Bandari ya Djibouti ili kuisafirisha kuja nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako