• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lahimizwa kuchukua hatua ili kuepusha hali ya Syria isizidi kuwa mbaya

    (GMT+08:00) 2018-04-12 16:51:05

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelihimiza Baraza la Usalama la Umoja huo lichukue hatua, ili kuepusha hali ya Syria isishindwe kudhibitiwa.

    Bw. Guterres ameeleza kusikitishwa kwake na kushindwa kwa Baraza la Usalama kuafikiana kuhusu shutuma za mashambulizi ya silaha za kemikali huko Ghuta nchini Syria. Amesisitiza kuwa Baraza hilo linapaswa kufanya juhudi na kumaliza mateso ya Wasyria.

    Habari nyingine zinasema, wizara ya mambo ya nje ya Syria jana iliilaani Marekani kwa kutishia kufanya operesheni ya kijeshi dhidi ya Syria. Imesema hatua hiyo ya Marekani ni ya kizembe na itaifanya hali ya Syria izidi kuwa mbaya.

    Na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang leo amesema China inaona wasiwasi na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Syria na kutoa wito kwa pande husika kujizuia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako