• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kutatua mzozo kuhusu mishahara ya wahadhiri

    (GMT+08:00) 2018-04-12 19:48:09

    Serikali imetakiwa kutatua mzozo kuhusu mishahara ya wahadhiri wa vyuo vikuu.

    Mvutano baina ya wahadhiri hao na serikali umetatiza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mwezi Mei, kutokana na mgomo wa wahadhri hao ambao sasa umeingia katika mwezi wake wa pili.

    Mzozo huo wa sasa umechochewa na kushindwa kwa wizara za elimu na fedha ,tume ya mishahara na marupurupu pamoja na jopo la pamoja la ushauri la vyuo vikuu kuwasilisha pendekezo mbadala kuhusu mishahara hiyo kama ilivyoagizwa na mahakama, ili kutoa fursa ya majadiliano kuhusu mishahara hiyo.

    Chama cha wahadhiri pamoja na kile cha wafanyikazi wa vyuo vikuu vimeapa kudumisha mgomo huo hadi matakwa yao yatakapo shughuilikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako