• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wapongeza msaada uliotolewa na China kwa wanafunzi wakimbizi wa Syria nchini Lebanon

    (GMT+08:00) 2018-04-13 09:02:32

    Shirika la Umoja wa mataifa la misaada ya dharura kwa watoto, limeipongeza China kwa msaada wake kwa wakimbizi watoto wapatao elfu 86 nchini Lebanon uliotolewa mwaka jana.

    Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Lebanon Bibi Tanya Chapuisat amesema hayo kwenye hafla ya kusainiwa kwa makubaliano ya kukamilisha msaada huo wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 1 kwa ajili ya kuiunga mkono wizara ya elimu ya Lebanon.

    Mwaka jana serikali ya China ililipatia shirika hilo msaada wa dola za kimarekani milioni 1, wenye lengo la kufanya watoto wote wanapata elimu, fedha ambazo zilitumika kutoa vifaa kwa ajili wanafunzi wakimbizi.

    Balozi wa China nchini Lebanon Bw Wang Kejian aliyehudhuria hafla ya makabidhiano hayo, amesema mradi umekamilika na msaada wote umekabidhiwa. Amesisitiza kuwa China itaendelea kuhimiza kuboresha hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako