• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana kudumisha msimamo wake kuhusu Rais Kabila wa DRC

    (GMT+08:00) 2018-04-13 10:01:19

    Waziri wa mambo ya nje wa Botswana Bw. Vincent Seretse amesema, serikali mpya inayoongozwa na rais Mokgweetsi Masisi haitabadilisha msimamo wake kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC hadi itakapofanya uchaguzi unaoaminika.

    Akiongea na wanahabari mjini Gaborone, Bw. Seretse amesema Botswana inaendelea kutoridhishwa na hali nchini DRC, na kumkosoa moja kwa moja rais Joseph Kabila wa DRC aliyekataa kufanya uchaguzi uliopangwa kufanyika kwa muda mrefu uliopita, na kusema hali hiyo ndiyo inayochochea vurugu na kusababisha msukosuko wa kibinadamu. Ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza shinikizo dhidi ya mamlaka ya DRC kuwalazimisha kuacha madaraka ili kutoa fursa kwa muundo mpya wa kisiasa.

    Habari zinasema hivi karibuni waandamanaji kadhaa nchini DRC wameuawa na baadhi ya mapadri walioshiriki kwenye maandamano wamekamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako